Thursday, April 26

Makaburi ya pamoja yagunduliwa Rwanda

Takriban watu laki nane waliuwawa ndani ya miezi mitatu.Haki miliki ya pichaAFP
Image captionTakriban watu laki nane waliuwawa ndani ya miezi mitatu.
Makaburi ya pamoja yamegundiliwa nchini Rwanda miaka 24 baada ya mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini humo.
Wenyeji wanaamini kuwa maeneo hayo yana maiti ya watu takriban elfu tatu.
Wakati ya mauaji wa kimbari mwaka 1994, zaidi ya watu laki nane waliuwawa ndani ya miezi mitatu.
Ugunduzi huo umekuja wiki moja baada ya muda ya maombolezi rasmi ya kukumbuka maafa makubwa ya dunia nchini humo. Watu wakujitolea wamekuwa mstari wa mbele katika kuchimbua makaburi hayo, baada ya kuambiwa kuhusu makaburi hayo na mwanamke mmoja alisema kwamba aliona miili hiyo ikitupwa hapo, zaidi ya miongo miwili iliyopita.
Ndugu wa walioathirika na mauaji ya kimbari wamekuwa wakutafuta ishara yoyote ya kuwabainisha kama wapendwao wao walizikwa katika eneo hilo.
Lakini ugunduzi huo umezua maswali mengi miongoni ya vyombo vya habari nchini humo ,je ni kwa nini watu waliofahamu kuhusu makaburi hayo hawakujitokeza mapema.
Baadhi waliohukumiwa kwa kutekeleza kimbari wamemaliza hukumu yao na kuachiliwa kutoka gerezani.

No comments:

Post a Comment