Thursday, April 26

Kutana na wataalamu wanaozunguka majumbani Zanzibar kupambana na Malaria

Habiba Suleima Seif, Ni afisa afya, Kitengo cha Kupambana na Malaria
Image captionHabiba Suleima Seif, ni moja wa maafisa wa afya, kitengo cha kupambana na Malaria Zanzibar
Leo ni siku ya kimataifa ya kupambana na ugonjwa wa Malaria. Kisiwa cha Zanzibar ni moja kati ya maeneo duniani yaliyofanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa malaria.
Kati ya watu 100 wanaopimwa damu kuangalia vimelea vya Malaria Zanzibar , haizidi zaidi ya mtu mmoja au chini ya asilimia moja anayekutwa na ugonjwa huo.
Mkurugenzi mtendaji wa kitengo cha kupambana na Malaria Zanzibar, Abdullah Suleiman anasema hiyo haina maana kwamba ugonjwa haupo, kwani kuna baadhi ya maeneo visiwani humo hali sio nzuri.
Zanzibar ni moja kati ya maeneo duniani yaliyofanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa malaria
Image captionZanzibar ni moja kati ya maeneo duniani yaliyofanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa malaria
Abdullah ameyataja maeneo hayo hususan katika wilaya ya Magharibi, Unguja kama vile Chukwani, Shakani, Wilaya ya Kati maeneo ya Cheju, na katika kisiwani cha Pemba ni maeneo ya kaskazini Pemba pamoja na Tumbe.
Mkuu huyo wa kitengo cha kupambana na Malaria Zanzibar, anaeleza kuwa mchanganyiko mkubwa wa watu, wengi wanaosafiri, kuna changia kiasi kikubwa maambukizo ya Malaria.
Mkurugenzi mtendaji wa kitengo cha kupambana na Malaria Zanzibar, Abdullah Suleiman
Image captionMkurugenzi mtendaji wa kitengo cha kupambana na Malaria Zanzibar, Abdullah Suleiman
''Watu wanatoka katika maeneo yenye malaria na kuja katika maeneo ambayo maambukizi yako chini sana, na kwa vile mbu wapo ni rasihi mbu kuchukua vimelea kwa mtu mwenye ugonjwa na kupeleka kwa asiye navyo'' amesema Abdullah Suleiman.
Ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika, hususan Afrika ya Mashariki, Zanzibar iko chini kwa maambukizo ya malaria, lakini Abdullah anasema mikakati na mbinu wanazotumia hazina tofauti na nchi nyingine kama vile utumiaji wa vyandarua, upigaji dawa katika nyumba, utafiti, elimu ya afya uchunguzi na matibabu.
Ameitaja siri ya mafanikio kuwa ni jamii kupokea kwa mwamko mkubwa kazi zote wanazozifanya kupambana na malaria.
Kumekuwa na utaratibi wa kugawa vyandarua majumbani
Image captionKumekuwa na utaratibi wa kugawa vyandarua majumbani
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, zaidi ya asilimia 85 ya watu wameweza kuyafuatilia kwa vitendo mapendekezo ambayo yanatolewa kupambana na ugonjwa huo.
Katika siku za hivi karibuni, Zanzibar pia imezindua tena vyandarua vyenye dawa kama juhudi zaidi kupambana na ugonjwa huo, hususan kwa wanawake wajawaziti na watoto walio na umri wa chini ya mwaka mmoja.
Utaratibi pia wa kugawa vyandarua unafanyika majumbani kupitia serikali za mitaa.

No comments:

Post a Comment