Tuesday, April 3

Magufuli: Tutarejeshewa sehemu ya anga iliyokasimiwa kwa Kenya

John MagufuliHaki miliki ya pichaIKULU, TANZANIA
Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli ameeleza matumaini kwamba taifa hilo litarejeshewa uangalizi wa sehemu ya anga lake ambayo kwa sasa huangaliwa na Kenya.
Hii ni baada ya rais huyo kuzindua ujenzi wa mitambo minne mipya ya rada.
Dkt Magufuli alisema hayo alipokuwa akimeweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa mfumo mmoja wa rada za kuongozea ndege katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere.
Shirika la Usalama wa Anga Duniani (ICAO) lilikasimu sehemu ya anga la Tanzania kwa Kenya kutokana na ukosefu wa mitambo ya kutosha Tanzania.
Dkt Magufuli amesema nchi hiyo imekuwa ikipoteza takribani Bilioni 1.2 ya tozo kwa mwaka kutokana na mpangilio huo.
"Hivi sasa Tanzania inapoteza takribani Bilioni 1.2 ya tozo kwa mwaka baada ya Shirika la Usalama wa Anga Duniani (ICAO) kukasimu sehemu ya anga la Tanzania kwa Kenya, baada ya mradi huu kukamilika tutarejeshewa sehemu hiyo," amesema Dkt Magufuli.
"Tanzania ina Rada moja tu iliyonunuliwa mwaka 2002 na ina uwezo wa kuhudumia anga kwa asilimia 25 tu lakini kukamilika kwa Rada hizi kutawezesha anga lote la Tanzania kuhudumiwa.
Dkt Magufuli ametoa wito kwa wanaotekeleza mradi huo kuusimamia vyema na kuhakikisha unakamilika „ndani ya muda au hata kabla ya muda wake"
"Mradi huu tunauhitaji haraka sana," amesema, na kutoa wito kwa raia nchini humo kuunga mkono juhudi za serikali yake katika kutekeleza miradi ya maendeleo.
"Miradi yote tunayotekeleza, ununuzi madawa, ndege zinazokuja yote hii ni yenu, sisi viongozi jukumu letu ni kusimamia utekelezaji wa miradi hii, Serikali ipo haijalala na haitalala."
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw Hamza Johari amesema: "Faida za mradi ni kuonekana kwa anga lote la Tanzania kwa asilimia 100 utakaosadia kuongeza usalama na mapato, pia mfumo huu utakuwa na uwezo wa kupanga ndege nyigi zaidi na unatarajiwa kutavutia ndege nyingi zaidi" .
Gharama za mradi ni bilioni 67.3 na zinafadhiliwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia 100 unaotarajiwa kuchukua miezi 18 kukamilika na utakamilika mwezi Mei 2019.
Mitambo hiyo minne itawekwa viwanja vinne vikuu vya ndege nchini humo: Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Mwanza, KIA Mkoani Kilimanjaro na Songwe, Mbeya
Tanzania baadaye leo ilipokea ndege ya tatu aina ya Bombardier Q400 kutoka Canada, ambayo ni kati ya ndege sita ambazo rais huyo aliahidi kununua kufufua shirika la ndege la taifa hilo.
Ndege ya tatu aina ya Bombardier Q400 ilipowasili uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius NyerereHaki miliki ya pichaMAELEZO.GO.TZ
Image captionNdege ya tatu aina ya Bombardier Q400 ilipowasili uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere
Ndege hiyo ilianza safari ya kuelekea Dar es Salaam mnamo Ijumaa wiki iliyopita.
Rais Magufuli, akiongea awali, alisema raia Tanzania wanafaa kujivunia hatua miradi ambayo inatekelezwa na serikali yake.
"Nchi ya Tanzania inaenda vizuri sana Watanzania watembee kifua mbele kwani nchi inakuwa kwa kasi, Ilikuwa ni aibu kwa nchi kubwa kama Tanzania kuwa haina ndege ya Serikali".

No comments:

Post a Comment