Friday, April 6

JPM atengua uteuzi wa mkurugenzi Mpwapwa



Katibu Mkuu wa Tamisemi, Mussa Iyombe 
Katibu Mkuu wa Tamisemi, Mussa Iyombe  
Dodoma. Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa mkurugenzi  wa halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa,  Mohamed Maje kuanzia leo Ijumaa Aprili 6, 2018 kwa kilichoelezwa kushindwa kutimiza majukumu yake.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Tamisemi, Mussa Iyombe leo imesema Maje ameisababishia Serikali hasara ikiwemo kushindwa hata kukusanya mapato ya Serikali.
"Hata makusanyo ya mwaka huu hatujui anapeleka wapi, hadi leo amekusanya asilimia 24 tu katika halmashauri kongwe kama Mpwapwa," amesema.

No comments:

Post a Comment