Wednesday, March 14

Wakili wa viongozi mtandao wa wanafunzi afunguka


Dar es Salaam. Wakili wa viongozi wa  Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Reginald Martine amesema wateja wake wameitwa kuhojiwa na mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ili kutoa ushahidi wa tukio la ‘kutekwa’ kwa mwenyekiti wao, Abdul Nondo.
Akizungumza na MCL Digital leo Machi 14, 2018, Martine amesema tayari viongozi wawili kati ya wanne wa mtandao huo wameshatoa ushahidi wao, kwamba hakuna vitisho vyovyote walivyopewa na polisi.
Amesema kuwa polisi wamemhakikishia kuwa hawatawashikilia viongozi hao na mara watakapomaliza kutoa ushahidi wataruhusiwa kuondoka.
“Utaratibu wa wakili mtu anapokuwa anatuhumiwa lazima uwe na mteja wako wakati anapohojiwa lakini kama mteja anatoa ushahidi wakili siyo lazima awepo hivyo wanaendelea kutoa ushahidi muda,” amesema.
Amesema walishauriana na  mmoja wa makamishna kuwa yeye asiwepo na viongozi hao wakati wanatoa ushahidi wao.
Waliofika kuhojiwa na  DCI ni mkaguzi wa haki za binadamu, Alphonce Lusako; katibu wa mtandao huo, Malekela Brigthon; ofisa habari Hellen Sisya na mkurugenzi wa Idara ya sheria, Paul Kisabo.
Waliokwisha hojiwa mpaka kufikia leo saa 7 mchana ni Lusako na Brigthon.

No comments:

Post a Comment