Friday, March 16

Waandishi watakiwa kuwa na umoja

Rais wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Jaji mstaafu Thomas Mihayo amewataka waandishi wa habari kuwa na umoja na kuaminiana na Serikali iliyopo madarakani ili kufikia lengo la kuwatumikia wananchi kwa pamoja.
Akizungumza Machi 15, 2018 katika hafla ya kuiaga na kuikaribisha Bodi mpya ya MCT jijini Dar esSalaam, Jaji Mihayo amesema tasnia ya habari inapita katika mawimbi makubwa ili kuyashinda inahitajika ushirikiano wa pamoja wa wadau wote.
Akizindua bodi hiyo, mgeni rasmi katika hafla hiyo, Mwandishi nguri, Hamza Kasongo amesema MCT imesaidia nchi kadhaa kushawishi kuanzishwa kwa Baraza la Habari.
Kasongo amesema kwa miaka miwili kuna vyombo vya habari vimefungiwa, kufutwa na vingine kutozwa faini kwa madai ya kutangaza habari ambazo hazikuwa na mizania.
Naye Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Bakari Machumu ambaye ni mmoja wa wajumbe wa bodi ya MCT amesema vyombo vya habari na Serikali, Bunge au Mahakama wanapaswa kuwa wadau wanaotegemeana kutokana na umuhimu wake kwenye jamii.
Amesema vyama mbalimbali vya habari na waandishi mmoja mmoja wanapaswa kutambua jukumu kubwa walilonalo la kuihudumia jamii.

No comments:

Post a Comment