Maelfu ya waandamanaji mara nyingine tena wamejitokeza Ijumaa katika mitaa ya miji ya nchi ya Slovakia kufuatia mauaji ya mwandishi wa habari za uchunguzi na mchumba wake wiki mbili zilizopita.
Waandamanaji hao wanataka kuwepo uchaguzi mpya na wanaelekeza hasira zao dhidi ya serikali.
“Ni lazima serikali iaachie madaraka. Ni kwamba watawala hao wameshikana pamoja, wote hao wanataka kuendelea kutawala katika nafasi zao,” mmoja wa waandamanaji Miroslav Sputsova aliuambia umati uliokusanyika siku ya Ijumaa jioni huko mji wa Bratislava.
Mauaji hayo ya mwandishi Jan Kuciak na mchumba wake, Martina Kusnirova yaliofanyika Februari 25, 2018 yameitikisa nchi ya Slovakia na nchi za Ulaya, ambako wasiwasi umeongezeka juu ya kuminywa uhuru wa habari na ukosefu wa usalama baada ya matukio kadhaa ya vitendo vya kuwadhuru wanahabari kutokea miezi ya hivi karibuni.
Washukiwa watatu wametuhumiwa kuhusika na mauaji ya Galizia. Lakini mara nyingi, haki imekuwa ikipindishwa, imesema ripoti..
Sheria zimeendelea kuwa kandamizi ulimwenguni na hali ya siasa kuwa tata baada ya vikundi vyenye pesa kuvidhibiti vyombo vya habari, wakizuia ujumbe na wakati mwengine kulazimisha ujumbe potofu kuwafikia wananchi, wanasema wachambuzi wa siasa huko Ulaya.
Na pengine juu ya yote hayo, wanadhani upo usaliti wa fikra nzima ya wananchi kulindwa na sheria na uhuru wa mahakama, Waandishi wa Habari wasio na mipaka wametahadharisha hilo katika ripoti yao.
Wameongeza kuwa katika baadhi ya maeneo ya Ulaya, na nchi nyingine ulimwenguni vyombo vya habari huru - na hivyo demokrasia yenyewe - iko hatarini
Wiki hii ujumbe wa wabunge wa Umoja wa Ulaya walitembelea nchi ya Slovakia katika shughuli maalum ya kutafuta ukweli juu ya hali ya demokrasia.
Umoja wa Ulaya umeeleza kuongezeka kwa wasiwasi juu ya suala zima la uhuru wa habari. Watu wanaohamasisha uhuru wa habari wanasema uminyaji wa demokrasia na vitisho vinaongezeka.
Serikali kandamizi zinaibuka kuanzia Uturuki na Urusi, na hivi sasa wimbi hilo linaelekea Slovakia, Jamhuri ya Czech ambako hivi sasa rais ameiita hadharani silaha feki ya Kalashnikov na kusema ‘hii ni kwa ajili ya waandishi wa habari.’
Pia ukandamizaji huo uko Bulgaria, na iliyokuwa Yugoslavia ya zamani,” amesema makamu rais wa Jumuiya ya Waandishi wa Habari Ulaya, William Horsley.
“Katika nchi zote hizo kandamizi, uvunjifu wa amani, kukosekana ulinzi wa raia, na ukandamizaji unaofanywa na vyombo vya serikali vinaendelea kila siku,” Horsley ameiambia VOA.
Mwezi Octoba 2017, Mwandishi wa habari wa nchi ya Maltese Daphne Caruana Galizia aliuwawa kwa kutegewa bomu katika gari lake. Mwanamke huyu alikuwa akichunguza ufisadi na alikuwa anakabiliwa na kesi kadhaa za kuwakashifu watu, moja wapo iliokuwa imefunguliwa na Waziri Mkuu Joseph Muscat.
No comments:
Post a Comment