Serikali ya Afrika Kusini imezitaja nyama za kusindika aina ya Polony kuwa zilikuwa na sumu iliyosababisha vifo vya watu 180. Na imewashauri watu kutotumia nyama yoyote ya kiwandani.
Amri hiyo imetolewa kwa wenye maduka kurudisha bidhaa hizo, na kuziondoa kabisa katika maduka yao.
Nchi zilizozuia uingizaji wa nyama hizo kutoka nchini Afrika ya Kusini ni pamoja na Namibia, Msumbiji, Malawi, Botswana, na Zambia.
Kenya nayo imepiga marufuku bidhaa za nyama kutoka Afrika Kusini. Kwenye taarifa iliyotumwa na mkurugenzi wa afya ya umma Kepha Ombcaho, wafanyabiashara wametakiwa kuacha kuagiza bidhaa za kampuni ya Enterprise Food Production na Rainbow Chicken.
Aidha agizo hilo limetaka wafanyabiashara kurejesha bidhaa ambazo tayari vilikuwa vimeagizwa.
Waziri wa kilimo na usalama wa chakula wa nchini Msumbiji amekaririwa kuwa wamiliki wote wa maduka yanayouza nyama hizo waanze kuziondoa mara moja kwenye maduka yao kutokana na hatari inayodhuru afya.
Wakati huo huo Kenya nayo imepiga marufuku bidhaa za nyama kutoka Afrika Kusini. Kwenye taarifa iliyotumwa na mkurugenzi wa afya ya umma Kepha Ombcaho, wafanyabiashara wametakiwa kuacha kuagiza bidhaa za kampuni ya Enterprise Food Production na Rainbow Chicken.
Aidha agizo hilo limetaka wafanyabiashara kurejesha bidhaa ambazo tayari vilikuwa vimeagizwa.
Imechukua zaidi ya mwaka mmoja kwa nchi ya Afrika kusini kugundua tatizo hilo.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters limesema kuwa Kumekuwepo na kesi 948 ya sumu ya Listeria nchini Afrika kusini ambalo Umoja wa Mataifa umeliita ni shambulizi kubwa kuwahi kutokea
Chanzo cha ugonjwa huo wenye sumu katika inaaminika kuwa umetoka katika kiwanda kilichopo Kaskazini mwa jiji la Polokwane, ambao unatengeneza vyakula vya aina mbalimbali.
Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Tiger, ambayo inamiliki viwanda hivyo alisisitiza jana kuwa "Hakuna uhusiano wowote" kati ya bidhaa anazozalisha na watu 180 waliokufa.
Kwa upande wake, Lawrence McDougall amesema kuwa kampuni yake walikuwa wametoa tahadhari ya kutazamwa upya kwa tangazo hilo la serikali.
Kampuni nyenza ya vyakula inayojulikana RCL nayo imekumbwa na tuhuma hizo hali iliyopelekea kusimamisha uzalishaji wa ayama.
Baada ya Mamlaka za Afya kuagiza kusitishwa kwa nyama hizo, maduka makubwa (supermarkets) ikiwemo Shoprite, Pick n Pay, Spar na Woolworths tayari zimeshaondoa bidhaa pamoja na hizo pamoja na bacon, na bidhaa nyingine za nyama za kusindikwa.
Baadhi ya wateja waliamua kurudisha bidhaa ambazo walikuwa wamenunua na kutaka kurudishiwa gharama zao.
Afisa mmoja wa Taasisi ya Taifa ya Magonjwa ya milipuko imeiambia gazeti la Times libe kuwa kumekuwepo na uhaba wa vipimo vinavyotumika kuangalia bakteria aina ya Listeria kwa muda wa wiki mbili katika kiwanda cha Polokwame
"Bakteria wa Listeria ni vigumu kugundulika kutokana na kujificha kwenye nyufa za viwanda"
Wateja waliokuwa wametunza bidhaa hizo aina ya Colony kwenye majokofu wameshauriwa kuziteketeza .
Listeria ni nini?
•Inaweza kupatikana kwenye vyakula vilivyobeba bacteria aina ya listeria au kuwa karibu katika mashamba ya wanyama
•Inaweza patikana kwenye chakula ambacho hakijapakiwa , ikiwa ni pamoja na Sandwich na Pate
•Dalili zake ni pamoja na kuwa na joto kali, mafua, kuhara na kutapika
•Watu walioathirika wanaweza wasionyeshe dalili zozote, lakini kwa wazee na vijana wanakuwa katika mazingira magumu zaidi
No comments:
Post a Comment