Tuesday, March 13

Trump amfuta kazi Waziri wa mambo ya nje Tillerson

Rex Tillerson in Chantilly, Virginia, October 5 2017Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMr Tillerson lasted in the job for just over a year
Rais wa Marekani Donald Trump amefukuza kazi Waziri wa mambo ya nje, Rex Tillerson na kumteua mkuu wa wa Shirika la Kijasusi, CIA, Mike Pompeo
Akimshukuru Bw Tillerson kwa huduma yake kupita akaunti yake ya Twitter, Bw Trump amesema Waziri mpya wa Mambo ya nje atafanya "kazi nzuri".
Bw Tillerson, aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya mafuta ExxonMobil, aliteuliwa kwenye kazi hio mwaka jana.
Rais Trump pia alimpendekeza Gina Haspel kuwa mwanamke wa kwanza kuwa mkuu wa CIA.
Wizara ya mambo ya ndani imesema Bw Tillerson hakuwa amezungumza na Rais na "hakufahamu sababu" za kutumbuliwa.
Akizungumza na waandishi wa habari nje ya White House siku ya Jumanne Bw Trump alisema tofauti baina yake na Bw Tillerson zilikuwa za "kibinafsi."
Afisa wa juu katika Ikulu ya Marekani, amezungumza na BBC kuhusu muda wa tangazo hilo kutolewa: "Rais alitaka kuhakikisha kuwa timu yake mpya kabla ya mkutano na Korea Kaskazini na baadhi ya mikutano mengine ya kibiashara"
Bw Tillerson alikuwa kwenye ziara rasmi ya Afrika wiki iliopita wakati ambapo alipata taarifa za ghafla za Trump kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.
KenyattaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionTillerson alipokutana na rais Uhuru Kenyatta
Katika juma moja ya ziara yake alitarajiwa kuzitembelea Chad, Djibouti, Ethiopia, Nigeria na Kenya ikiwa ni ziara yake ya kwanza barani Afrika.
Siku ya Jumamosi ,msemaji wake alisema amesitisha shughuli alizokuwa anapaswa kufanya nchini Kenya kutokana na hali yake ya kiafya kutokuwa nzuri.

No comments:

Post a Comment