Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Machi 10, 2018 inaeleza kuwa hitilafu hiyo imesababisha kukosekana kwa huduma ya umeme katika maeneo na mikoa yote iliyoungwa kwenye gridi hiyo.
Inaeleza kuwa baada ya hitilafu hiyo kutokea, mafundi na wataalamu wamechukua hatua za haraka na bado wako kazini kuhakikisha kuwa umeme unarejea mapema kadri iwezekanavyo.
“Uongozi wa shirika unaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza. Tafadhali usishike wa kukanyaga waya ulioanguka au uliokatika, ukiuona toa taarifa,” inaeleza taarifa hiyo.
No comments:
Post a Comment