Wednesday, March 14

Kampuni yashusha bei ya mbolea ya kupandia


Dar es Salaam.Katika kuunga mkono jitihada za Serikali kuhakikisha wakulima wanapata mbolea kwa wakati na gharama nafuu, kampuni ya uzalishaji na usambazaji wa mbolea ya Yara imeshusha bei ya mbolea ya kupandia.
Mbolea hiyo ya chumvi chumvi inayofahamika kama Yara Mila Otesha imepungua bei kwa asilimia 50.
Ofisa masoko wa kampuni hiyo, Linda Byaba amesema leo Machi 14, 2018 kuwa uamuzi wa kupunguza bei umekuja ili kuwasaidia wakulima waweze kupata mbolea kwa gharama nafuu.
Amesema mbolea hiyo ina virutubisho muhimu vinavyosaidia mazao kuzalishwa kwa wingi.
Amesema virutubisho vilivyo ndani ya mbolea hiyo ni lishe linganifu kwa mmea na husaidia katika kuchochea uotaji wa mizizi.
“Mbolea hii inasaidia sana kuufanya mmea kuwa imara,” amesema.

No comments:

Post a Comment