Tuesday, March 6

Afya ya Mbowe yazidi kuimarika


Moshi. Afya ya mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliyeruhusiwa jana kutoka Hospitali ya Rufaa ya KCMC baada ya kulazwa kwa saa 24 inazidi kuimarika.
Akizungumza leo Jumanne Machi 6, 2018 katibu wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema amesema Mbowe ambaye pia ni mbunge wa Hai kwa sasa anaendelea vizuri na yuko kwenye mapumziko.
"Tunamshukuru Mungu mwenyekiti anaendelea vizuri sana kwa kweli. Kwa sasa yupo katika mapumziko,” amesema Lema.
Mbowe, ambaye jana Machi 5, 2018 alipaswa kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam, aliugua ghafla juzi usiku akiwa anapata chakula na viongozi wengine katika hoteli ya Keys mjini Moshi kabla ya kuwahishwa KCMC kwa matibabu.

No comments:

Post a Comment