Akizungumza leo Jumatatu Desemba 4,2017 IGP Sirro amesema walisaini makubaliano ya kufanya operesheni kwa pamoja kukomesha uhalifu na kubadilishana wataalamu.
Amesema kuna wataalamu kutoka Rwanda watatoa mafunzo ya kushughulikia makosa ya kimtandao.
“Wenzetu wa Rwanda ni wazuri kwenye masuala ya kudhibiti uhalifu wa kimtandao, hivyo watatoa mafunzo kwa wataalamu wetu,” amesema IGP Sirro.
Amesema wamepata mafanikio kwa kushirikiana na Rwanda kwa kukamata dawa za kulevya zikiwemo bangi mkoani Kagera na wameimarisha usalama katika ukanda wa kati.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Rwanda, Casana amesema tangu wameingia mkataba huo wamekuwa wakibadilishana wataalamu kwa ajili ya kupeana mafunzo.
No comments:
Post a Comment