Minda Mfamai na mkewe Fatuma Mpondi ambao ni wafanyabiashara wamepandishwa kizimbani pamoja na mwenzao Oswini Mango wakidaiwa kusafirisha gramu 375.20 za dawa za kulevya aina ya heroin.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri; wakili wa Serikali, Adolf Mkini amedai Novemba 22,2017 katika maeneo ya Chamazi kwa Mkongo, Dar es Salaam washtakiwa walisafirisha dawa hizo.
Baada ya kusomewa shtaka leo Jumanne Desemba 5,2017 washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu chochote kwa sababu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo isipokuwa Mahakama Kuu.
Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi Desemba 19,2017.
Mahakama imeamuru mshtakiwa Minda akatibiwe baada ya kulalamika kuwa alipigwa akiwa polisi.
No comments:
Post a Comment