Wednesday, December 6

Upelelezi wa mfanyabiashara aliyekamatwa Z’bar bado


Imeelezwa kuwa mfanyabiashara aliyekamatwa kwa tuhuma za kukutwa na vito vya dhahabu na mamilioni ya fedha ya nchi 15 ataendelea kuwa chini ya ulinzi hadi uchunguzi dhidi yake utakapomilika.
Naibu Mkurungezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar, Ramadhani Ng’anzi alisema juhudi za ukamilisha uchunguzi dhidi ya tukio hilo zinaendelea.
“Hatuwezi kusema wapi tumefikia hadi pale tutakapokamilisha kazi yetu ya uchunguzi, ila tunaendelea kumshikilikia kwa mujibu wa taratibu zetu,” alisema Ng’anzi.
Kaimu Kamishna wa Polisi Zanzibar, Juma Yussuf Ali alisema mfanyabiashara huyo alikamatwa baada ya kutiliwa shaka wakati akitaka kusafiri nje ya nchi.
Ali alisema kwa mujibu wa taratibu za kipolisi na kiusalama ililazimika kumzuia mfanyabiashara huyo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa mali alizotaka kuondoka nazo nje ya nchi.
Msemaji wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar, Makame Abdalla alisema kukamatwa kwa mfanyabiashara huyo uwanjani hapo ni tukio kubwa la kwanza kutokea.

No comments:

Post a Comment