Saturday, December 2

Ujumbe wa al-Qaeda unaonyesha mpasuko baina vikundi vya jihadi




Mpiganaji wa al-Qaeda nchini Syria
Kikundi cha kigaidi cha al-Qaida kimetoa ujumbe mpya wa sauti ya kiongozi asiyetabirika ambaye analikosoa kundi la wapiganaji Jihadi wa Syria lijulikanalo kama Liberation of the Levant Organisation.
Kundi hilo pia linajulikana kwa jina jingine maarufu Hayat Tahrir al-Sham (HTS), na kiongozi wa al- Qaeda anawalaumu kwa kuwashambulia wapiginaji jihadi waandamizi wenye mafungamano na al-Qaeda huko Syria.
Katika sauti ya video hiyo ya dakika 35 “Ayman al-Zawahiri anasema na tupigane nao kwa msimamo moja, wakati akipinga uamuzi wa HTS kusitisha mafungamano rasmi na al-Qaeda 2016 na kutoweka ahadi yao ya mafungamano ya pamoja kama ni sehemu ya kikundi cha kigaidi ndani ya Syria. Sauti ya Amerika,VOA, haikuweza kuthibitisha ukweli wa video hiyo.
“Kwa nini upendo huu umepotea kati yetu na umerithiwa na migogoro, ukatili wa mioyo, njama za kuvunja kiapo chetu cha ushirikiano, na kuwadharau ndugu zetu na kutaka kuwaondoa nchini, kuwazuilia na hata kuwateka?
Al-Zawahiri amesema hayo alipokuwa anawahutubia viongozi wa HTS katika ujumbe wake, uliokuwa umeandikwa katika vyombo vya habari vya al-Qaeda vinavyofanyapropaganda vya al-Sahab Foundation Jumanne.
HTS ambayo mwanzoni ilikuwa inajiita al-Nusra Front, ilijibadilisha mwaka jana na baadae kuungana na vikundi kadhaa vidogo vya upinzani na kuunda umoja wao.
Ripoti iliyoandaliwa na Taasisi ya utafiti wa kivita wiki iliyopita imedai kuwa kikundi hicho imetumia fursa ya hatua ya jumuiya ya kimataifa kukishinda kikundi cha Islamic State kama ni nafasi ya kuongeza kwa kiwango kikubwa himaya yake upande wa Kusini mwa Syria, ikiimarisha udhibiti wa maeneo mengi ya kaskazini mashariki ya jimbo la Idlib.
Al-Zawahiri amesema yeye hakuidhinisha kujitoa kwa kikundi cha HTS kutoka katika mtandao wa al-Qaida. Anaelezea kuwa ni “kosa kubwa sana” walilofanya viongozi wa HTS kufanya ushirikiano wao naye kuwa siri kwa ajili ya kuepuka mashambulizi ya majeshi yanayoongozwa na Marekani.
Mnamo August, Michael Ratney, afisa wa ngazi ya juu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ambaye anashughulikia sera ya Syria, amesema kikundi cha Nusra na viongozi wake watakuwa ni walengwa wa Washington hata kama watajibadilisha na kutumia majina mapya kwa ajili ya kuepuka mashambulizi ya majeshi ya Marekani na nchi nyingine yanayopambana kuutokomeza ugaidi katika eneo hilo.

No comments:

Post a Comment