Friday, December 1

Harufu mbaya ya soksi yamtia abiria matatani India

Picha ya kuashiriaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Polisi nchini India wanasema wamemkamata mwanamume mmoja ambaye uvundo wa soksi zake ulisababisha ugomvi kati yake na abiria wenzake kwenye basi.
Waliambia BBC kwamba wamewasilisha kesi dhidi ya Prakash Kumar, 27, kwa "kuvuruga amani ya umma".
Kisa hicho kilitokea kwenye basi lililokuwa safariki kuelekea mji mkuu Delhi, baada ya Kumar kuvua viatu vyake na soksi.
Harufu mbaya kutoka kwenye soksi zake ilikuwa mbaya sana kiasi kwamba abiria walimuomba Bw Kumaru kuziweka ndani ya mkoba wake au kuzirusha nje ya basi.
Lakini anadaiwa kukataa hilo, na ugomvi mkali ukazuka.
Abiria kisha walimlazimisha dereva wa basi hilo kuingia kituo cha polisi katika jimbo la Himachal Pradesh, kaskazini mwa India, ambapo malalamishi dhidi yake yaliwasilishwa.
Gazeti la Hindustan Times limemnukuu Bw Kumar akisema kwamba soksi zake hazikuwa na harufu mbaya, na kwamba abiria wenzake waligombana naye "bila sababu".
Polisi wameambia BBC kwamba mwanamume huyo amepewa dhamana.

No comments:

Post a Comment