Afisa wa masuala ya siasa wa umoja wa Mataifa anaanza ziara isiyo ya kawaida wa siku nne huko Pyongyang siku ya Jumanne
Ziara hiyo ya Jeffrey Feltman ndiyo ya kwanza kufanywa na afisa wa cheo cha juu wa Umoja wa Mataifa katika kipindi cha miaka sita.
Korea Kaskazini ilikuwa imetoa mwalika kwa Umoja wa Mataifa mwezi Septemba kufanya ziara.
Ziara hii inakuja baada ya jaribio la wiki iliyopita ambalo Korea kaskazini ilidai kuwa ndilo lenye nguvu zaidi la masafa marefu ikidai kuwa linaweza kushambulia Marekani.
Bw. Feltman, mwanadiplomasia wa zamani wa Marekani na afisa wa cheo cha juu zaidi kufanya kazi na Umoja wa Mataifa atakuwa mjini Pyongyang hadi Ijumaa.
Ziara yake inakuja wakati Korea Kusini na Marekani wanafanya mazoezi makubwa zaidi ya agani kuwai kufanywa.
China ambayo ni mshirika wa jadi wa Korea Kaskazini na mshirika mkubw wa kibiashara ilimtuma mwanadiplomasia wa cheo cha juu kwenda Korea Kaskazini mwezi uliopita kwa majadiliano na maafisa huko.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa hakuna mipango kwa sasa kwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye amejitolea kuwa mpatanishi kwenye mzozo wa Korea Kaskazini kuzuru nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment