Watu nchini Zimbabwe wanasubiri kuona hatua ambazo jeshi litachukua baada ya kutwaa madaraka ya nchi hiyo.
Rais Robert Mugabe yuko katika kizuizi cha nyumbani mjini Harare lakini ripoti ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa mke wake Grace ambaye alikuwa anataka kumrithi akimekimbia kwenda Namibia
Hatua za kijeshi zilifuatia kufutwa kwa Makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa ambayr ni hasimu mkubwa wa Bi Grace Mugabe.
Mahala alipo Mnangagwa pia hapajulikani.
Lakini mzozo kuhusu ni nani anaweza kumrithi Mugabe kati ya Bi Grace Mugabe na Bwa Mnangagwa umekigawanya chama cha Zanu-PF miezi ya hivi karibuni.
Nchi za Jumuia ya maendeo ya kusini mwa Afrika (SADC) zinatarajiwa kufanya mkutano wa dharura nchini Botswana leo Alhamisi.
Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe Tendai Biti, aliiambia BBC kuwa anataka kuona serikali ya mpito madarakani.
Siku ya Jumatano wanajeshi wakiwa na magari ya jeshi walilizinga bunge na majengo mengine makuu ya serikali.
Saa kadha baadaye walichukua udhibiti wa makao ya kituo cha habari cha serikali ZBC na kutangaza kuwa walikuwa wanawalenga waalifu wanamzunguka Rais Mugabe.
Hata hivyo meja Jenerali Sibusiso Moyo alikana kuwa hakkukuwa na mapinduzi wa kijeshi.
Alisema kuwa Mugabe na familia yake walikuwa salama.
No comments:
Post a Comment