Akizungumzia kutokea kwa ajali hiyo leo Jumapili, mwenyekiti wa kijiji cha Kikavu chini, Swaleh Msengesi amesema gari hilo lilikuwa limebeba watu hao waliokua katika mkesha wa kuhamasisha wapiga kura usiku wa kuamkia leo Jumapili.
Miongoni mwa waliojeruhiwa katika ajali hiyo ni Sakra Mtenga ambaye ni mjumbe wa Baraza Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Hai, Veronika Mmboga ambaye ni Diwani Vitu Maalum Same na Sophia Sharikiwa, ambaye ni Diwani Viti Maalumu Mwanga.
"Wote wamepelekwa katika hospitali ya Mkoa ya Mawenzi," amesema mwenyekiti huyo.
No comments:
Post a Comment