Sunday, November 26

Gari la Naibu Meya lashambuliwa


Iringa. Gari la Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa, Dadi Igogo limeshambuliwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa CCM.
Igogo amesema watu waliohusika na tukio hilo anawafahamu na tayari ametoa taarifa polisi ili waweze kuchukukiwa hatua.
Akizungumza na Mwananchi leo Jumapili, Igogo amesema amekumbwa na kadhia hiyo saa  sita mchana wakati alipotembea vituo vya kupiga kura.
"Nilikuwa natembelea vituo vya kupiga kura kuona zoezi linavyoendelea, ghafla gari langu likashambuliwa kwa mawe na watu ninaowafahamu," amesema Igogo.
Kamanda wa polisi mkoani hapa, Julius Mjengi alipoulizwa kuhusu tukio hilo hakuthibitisha wala kukataa na badala  yake ametaka mwandishi kuvuta subira.
"Kuhusu jambo hilo subiri kidogo,” amesema
Kuhusu upigaji kura amesema unaendelea vizuri katika mitaa yote 23 linakofanyika zoezi hilo la kupiga kura.

No comments:

Post a Comment