Mwaka 2013, Serikali iliweka lengo la kuwafanyia tohara wanaume milioni tatu ifikapo mwaka 2015.
Akizungumzia kampeni hiyo juzi, mratibu wa tohara Kanda ya Ziwa wa Shirika la Intra Health Tanzania, Paul Mwakipesile alisema watafanya upimaji kabla ya kumfanyia tohara mhusika kwa sababu asilimia 60 ya kufanya tohara hupunguza maambukizi ya Ukimwi.
Mwakipesile alisema wamepanga kuwafikia wanaume 71,495 katika wilaya zote za Simiyu, huku ikitarajiwa Itilima watafikiwa wanaume 26,000.
“Mwaka huu tutafikia malengo yetu kwa asilimia 100 katika vituo vya afya, maeneo yenye uhitaji tunaihusisha jamii. Tunafanya upimaji, tunatoa kondomu na tunafundisha uzazi wa mpango,’’ alisema.
Naye mratibu wa Ukimwi mkoa wa Simiyu, Dk Hamis Kulemba alisema kwa mwaka 2016 walipanga kufanya tohara kwa wanaume 42,000, lakini waliwafikia 38,000 sawa na asilimia 91.
Akizungumzia kampeni hiyo, mkuu wa mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka aliwataka wakazi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa hiyo.
No comments:
Post a Comment