Serengeti. Washtakiwa tisa waliokuwa wakikabiliwa na kesi nne tofauti za kukutwa na nyara za Serikali zenye thamani ya zaidi ya Sh107 milioni, wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kila mmoja.
Hakimu mkazi mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Serengeti, Ismael Ngaile alitoa hukumu baada ya kuwatia hatiani washtakiwa kwa makosa ya kukutwa na meno ya tembo, mafuta ya simba, mikia ya nyumbu, nyama ya ngiri, swalapala na ngozi ya nyati. Washtakiwa wawili waliachiwa.
Waliohukumiwa ni Mniko Masero (28), Silasi Ndarawa (26), Chacha Wambura (39), Jonas Mturi (45), Maseboka Mavuno (47), Nyaibane Nyaronge (29), Hinga Marwa (32), Ikwabe Marwa (36) na Josephat Luharamagara (42).
Awali, wakili wa Serikali Emmanuel Zumba aliieleza Mahakama kuwa Desemba 19, 2016 washtakiwa walikamatwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
No comments:
Post a Comment