Profesa Mwakalila amesema hayo leo Novemba 3 wakati alipozungumza na wanafunzi waliojiunga na chuo hicho mwaka huu ikiwa ni kuwakaribisha na kuwapatia maelekezo na taratibu za chuo.
Amesema kipindi hiki siyo cha kujihusisha wala kukubali kutumika na wanasiasa kwani ndoto zao zinaweza kuishia njiani na kupoteza dira.
“Sisi hatuwaruhusu wanafunzi wetu kujihusisha na masuala ya kisiasa au kutumika kwani tunaona vyuo vingine vinavyokumbwa na mambo kama hayo kwetu ikibainika sheria kali zitachukuliwa dhidi ya mwanafunzi atakaye husika,”amesema Profesa Mwakalila.
Amesema ikiwa baadhi ya vyuo wanafunzi wake kujihusisha na masuala ya siasa inasababisha migomo na maandamano yasiyo na tija wakati wa kudai haki zao.
Profesa Mwakalila amebainisha kwamba katika chuo hicho kuna utaratibu maalumu kwa wanafunzi kuwasililisha hoja zao kupitia serikali ya wanafunzi ambayo inaingia moja kwa moja katika maamuzi ya bodi na taasisi kwa ujumla.
“Kama kuna malalamiko yeyote taasisi yetu imejikita katika kutafutia ufumbuzi na kushirikiana moja kwa moja na Serikali ya wanafunzi katika kutolea ufafanuzi,”amesema Profesa Mwakalila.
Mbali na hilo mkuu huyo alibainisha changamoto iliyopo ya ni nyumba za kulala wanafunzi ambao wengi wao wanaishi nje na wanapendelea kuishi ndani ya chuo hicho lakini kuna utaratibu ambao wameweka kama chuo.
“Mabweni tuliyonayo ni machache kuna ambayo yanamilikiwa na watu binafsi kwa makubaliano ya kuweka bei elekezi kwa wanafunzi na miundombinu ambayo inaridhisha,”amesema Profesa Mwakalila.
Profesa Mwakalila amewatoa hofu wanafunzi wa ngazi mbalimbali kuanzia Astashahada, stashahada na shahada kuwa na amani na utulivu na watapatiwa elimu ambayo itakuwa na tija katika soko la ajira na kujenga uchumi wa taifa.
Mmoja wa wanafunzi waliojiunga na chuo hicho mwaka huu Stela Martin amesema anafurahi kupata nafasi ndani ya chuo hicho na kwamba maelekezo waliyoyapata yatawasaidia kuwajenga na kuwaandaa kuwa viongozi hodari.
No comments:
Post a Comment