Sunday, November 5

Waliomshambulia mgombea udiwani kufikishwa mahakamani


Wafuasi 12 wa Chadema waliokamatwa juzi usiku Kwa kosa la kumshambulia mgombea wa udiwani wa kata ya Muriet, Francis Mbise wanatarajia kufikishwa mahakamani kesho.
Wafuasi hao akiwemo Kaimu Katibu wa Chadema wilayani Arusha, Innocent Kisanyage  walishikiliwa juzi na polisi eneo la FFU Kwa Morombo wakidaiwa kumshambulia mgombea huyo sehemu mbalimbali za mwili wake.
Mbali na polisi kuwashikilia wafuasi hao pia gari la matangazo linalotumika katika mikutano mbalimbali ya kampeni lilishikiliwa.
Akizungumza na waandishi wa habari Leo Novemba 5 Kamanda Polisi mkoani Arusha (RPC), Charles Mkumbo amesema kwamba wafuasi hao wote 12 watafikishwa mahakamani kesho.
Hata hivyo, Kamanda Mkumbo alipoulizwa kuhusu gari la matangazo lililoshikiliwa siku ya tukio hakuweza kukiri au kukataa endapo wameliachia gari hilo na kufafanua kwamba wao hawana shida na gari hilo.
"Sisi tumekamata watu na hatuna shida na gari la matangazo kwani tumekamata watu au gari" amesema Mkumbo

No comments:

Post a Comment