Sunday, November 26

Wagombea Chadema wajitoa Arusha


Arusha. Wagombea udiwani wawili wa Chadema mkoani Arusha wametangaza kujitoa kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi mdogo unaofanyika leo Jumapili katika Kata ya Maroroni na Embuleni.
Wagombea hao ni Asanterabi Lazaro(Maroroni) na Dominick Mollel (Embuleni).
Wakizungumza na Mwananchi  wagombea wamesema  hawana sababu ya kuendelea na uchaguzi  uliotawaliwa na vurugu na hujuma.
Mbise amesema mawakala wake wamezuia kuingia vituoni na wengine kukamatwa.
Kwa upande wake mgombea wa Embuleni, Mollel alisema anajitoa kwani uchaguzi sio huru na haki.
"Tutaenda mahakamani kudai haki huu sio uchaguzi ni vita," amesema.

No comments:

Post a Comment