Thursday, November 2

Viwango vya ajali vyashuka kwa asilimia 48 Tanzania

Ajali ya barabarani iliofanyika nchini India. Nchini Tanzania viwango vya ajali kama hizo vimeshuka kwa asilimia 48
Image captionAjali ya barabarani iliofanyika nchini India. Nchini Tanzania viwango vya ajali kama hizo vimeshuka kwa asilimia 48
Ajali za barabarani zimepungua kwa asilimia 48 katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka 2017 ikilinganishwa na kipindi kama hicho 2016 kwa mujibu wa mkuu wa idara ya trafiki nchini Tanzania Fortunatus Musilimu.
Kwa mujibu wa gazeti la The Citizen nchini Tanzania, Kulingana na ripoti ya maafisa wa polisi, ajali za barabarani zilishuka kwa 1,264 ambayo ni asilimia 48.
Hii ni kutoka 2,639 zilizorekodiwa 2016 hadi 1,375 mwaka huu.
Kulingana na afisa huyo vifo na majeraha yalishuka kwa 239 ambayo ni asilimia 32 na 974 ambayo ni asilimi 40 mtawalia.
Akizungumza na waandishi habari wakati wa uzinduzi wa wiki ya usalama barabarani, alisema kuwa kushuka kwa viwango hivyo kunatokana na juhudi za idara ya polisi wa trafiki, iliotilia mkazo sheria za trafiki mbali na kuhamasisha madereva na uma kuhusu sheria hizo.
''Tumekuwa tukitoa hamasa kupitia mipango kadhaa ikiwemo ule wa wiki ya usalama barabarani.Pia ninawaahidi kwamba nitawachukulia hatua madereva wanaokiuka sheria za barabarani'', alisema.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, Bwana Musilimu aliwaalika watuamiaji wote wa barabara katika kampeni ya usalama barabarani inayotarajiwa kuanza tarehe 18 hadi 25 Novemba mwaka huu katika mji wa Dar es Salaam.
Amesema kuwa baada ya kampeni hiyo , idare'a ya polisi haitowavumilia wakiukaji wa sheria hizo wanaodai kutozijua.

No comments:

Post a Comment