Thursday, November 2

Papa Francis akiri kushikwa na usingizi wakati anapofanya maombi

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani papa Francis amekiri kwamba mara nyengine yeye hushikwa na usingizi wakati anapoombaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionKiongozi wa kanisa katoliki duniani papa Francis amekiri kwamba mara nyengine yeye hushikwa na usingizi wakati anapoomba
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani papa Francis amekiri kwamba mara nyengine yeye hushikwa na usingizi wakati anapoomba.
''Wakati ninapoomba , mara nyengine mimi hushikwa na usingizi'', alisema katika kipindi kimoja cha kanisa hilo cha TV2000 kilichochapishwa katika mtandao wa You tube.
''Mtakatifu Theresa pia alikuwa akilala'', alisema kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 80 kuhusu mtakatifu huyo wa karne ya 19.
Lakini akasema kuwa kushikwa na usingizi wakati wa maombi huwa ''kunamfurahisha mungu na kwamba Wakristo walitakiwa kuhisi kama watoto wanaolalia mkono wa baba yao''.
Ripoti zinasema kuwa papa Francis hulala mwendo wa saa tatu na kuamka saa kumi alfajiri kila asubuhi

Mtoto amvua kofia Papa Francis
Raia huyo wa Argentina amekuwa kiongozi wa kanisa katoliki tangu 2013 na amekuwa na ratiba ilio na mambo mengi ya ziara za kigeni na mikutano ya kuonekana hadharani.
Amekuwa maarufu kwa baadhi ya mabadiliko na uwazi katika uongozi wake hususan katika utumizi wa lugha ya moja kwa moja inayoeleweka.

No comments:

Post a Comment