Wednesday, November 29

Urusi yapoteza mawasiliano na satelaiti yake baada ya kuizindua

Setlait ya ta hali ya hewa ya urusi baada ya kuzinduliwa
Image captionSatelaiti ya hali ya hewa ya Urusi baada ya kuzinduliwa
Urusi imepoteza mawasiliano na satelaiti yake ya hali ya hewa saa chache baada ya kuizindua.
Mawasiliano yamepotea kwa sababu haiko katika mzingo wak , kulingana na shirika la angani la Roscoms.
Satelaiti hiyo kwa jina Meteor-M ilibebwa katika roketi ya Soyuz.
Uzinduzi huo ulifanyika kutoka eneo la Vostochny cosmodrome mashariki mwa Urusi.
Ni uzinduzi wa pili kutoka kambi hiyo ambayo ilifunguliwa mwaka uliopita.
Satelaiti ndogo pia zilikuwemo.

No comments:

Post a Comment