Wednesday, November 29

Samia amtembelea Lissu hospitali

Nairobi-Kenya. Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan leo Jumanne Novemba 28, 2017 amemtembelea mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu aliyelazwa Hospitali ya Nairobi nchini hapa.
Msafara wa Samia umefika hospitalini hapa saa 11.43 jioni akiwa  ameambatana na Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk Pindi Chana.
Mwananchi lililokuwapo hospitalini hapo wakati Mama Samia, Balozi Chana  na maofisa wengine wakiwasili hospitalini hapo.
Lissu amelazwa hospitalini hapo akiuguza majeraha ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 aliposhambuliwa Septemba 7 akiwa nyumbani kwake, Area D mjini Dodoma.
Makamu wa Rais amefika hospitalini akiwa njiani kurudi Tanzania baada ya asubuhi kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Rais Uhuru Kenyatta.
Samia anakuwa kiongozi mkuu wa kwanza wa Serikali ya Tanzania kumtembelea Lissu hospitali tangu alipolazwa usiku wa Septemba 7.

No comments:

Post a Comment