Friday, November 3

Upelelezi kesi ya Kitilya na wenzake bado haujakamilika


Dar es Salaam. Mwenyekiti wa kampuni inayoshughulikia  uwekezaji wa mitaji na dhamana (Egma), Harry Kitilya na waliokuwa maofisa wa benki ya Stanbic, Shose Sinare na Sioi Solomon bado wanaendelea kusota rumande kutokana na upelelezi wa kesi inayowakabili  bado haujakamilika.
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi ameeleza mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa  leo Ijumaa kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
Pia ameeleza kuwa bado wanasubiri awamu ya pili ya upelelezi kutoka nchini Uingereza, kutokana na hilo ameomba kesi hiyo ipangiwe tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.
Baada ya ombi hilo Hakimu Mwambapa ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 10, 2017 kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.

No comments:

Post a Comment