Friday, November 3

Nape amshangaa Nyalandu kubadili imani


Dar es Salaam. Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye amembeza aliyekuwa mbunge wa Singida Kaskazini (CCM), Lazaro Nyalandu kwa kujivua uanachama wa chama hicho na kuonyesha dhamira ya kujiunga na Chadema.
Nape aliyewahi kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amekuwa mbunge wa pili wa CCM kuzungumzia uamuzi wa Nyalandu akitanguliwa na mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde ‘Kibajaji.’
Kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Twitter, Nape ameandika ujumbe ukiambatana na picha inayowaonyesha yeye, Nyalandu na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana wakiwa na nyuso za tabasamu.
Ujumbe huo ulisomeka “Chama cha siasa ni itikadi, itikadi ni imani, siamini sana katika kubadili imani kienyeji. Nitashughulikia mapungufu nikiwa ndani sio nje!”
Akichangia hoja hiyo ya Nape, Amarison Tanga amesema, ‘’hapo ndipo ninapokukubali kiongozi wangu.
Kulwa Ngwembe‏ yeye amesema ‘’utasukumaje gari ukiwa ndani yake? Hicho chama ni gari bovu shuka chini.”

No comments:

Post a Comment