Friday, November 3

''Ugonjwa unaodaiwa kuwaua watoto wengi Afrika''

Maafisa wa matibabu wameanzisha kampeni ya kuwepo kwa chanjo ya gharama ya chini kukabiliana na ugonjwa huo
Image captionMaafisa wa matibabu wameanzisha kampeni ya kuwepo kwa chanjo ya gharama ya chini kukabiliana na ugonjwa huo
Takriban watoto milioni moja hupoteza maisha yao kutokana na homa ya mapafu licha ya kuwa inaweza kutibiwa kwa kutumia dawa za antibiotics ambazo hugahrimu chini ya dola moja imesema ripoti ya shirika la save the Children.
Ikielezea ugonjwa huo kama uliosahaulika, inasema kuwa ugonjwa huo umewaua watoto wengi chini ya miaka mitano zaidi ya ugonjwa wowote ule na eneo la jangwa la sahara limepiga hatua chache katika kukabiliana na vifo hivyo.
Nigeria, DR Congo , Ethiopia na Angola zina idadi kubwa ya vifo ya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano kutokana na homa ya mapafu pamoja na India na Pakistan.
Wengi wanaofariki ni watoto waliopo chini ya amiaka miwili , wengi wakiwa na kinga dhaifu iliokabiliwa na ukosefu wa chakula bora , ripoti hiyo imeongezea.
Shirika la save The Children limetoa wito wa kifanyika kwa mkutano wa viongozi duniani kutathmini tatizo hilo la homa ya mapafu.
Pia linataka kinga za gharama ya chini, kuwepo kwa dawa na zaidi ya watoto milioni 160 wapatiwe chanjo.

No comments:

Post a Comment