Mwanasheria mkuu nchini Saudi Arabia amesema takriban dola bilioni 100 zilifujwa kwenye ufisadi na matumizi mabaya ya fedha miongo ya hivi karibuni.
Sheikh Saud al-Mojeb alisema kuwa watu 199 wanazuiliwa kuhojiwa kama sehemu ya hatua kubwa ya kupambana na ufisadi ambayo ilianza Jumamosi usiku.
- Wana wa ufalme wakamatwa Saudi Arabia
- Hoteli ya kifahari ambayo ni gereza kwa wanawafalme Saudi Arabia
Hakumtaja yeyote lakini wanaripotiwa kuwa mingoni mwao wanawafalme wa vyeo vya juu, mawaziri na wafanyabiashara maarufu.
"Ushahidi wa uaovu uliotendeka ni mkubwa sana," Sheikh Mojeb alisema.
Alisema kuwa shughuli za kawaida katika ufalme huo hazijaathiriwa na kukamatwa kwa watu hao na akaunti binafsi za benki zilizofungwa.
- Mwanamfalme wa Saudi Arabia afariki katika ajali ya ndege
- Saudi Arabia yailaumu Iran kwa kombora lililorushwa Riyadh
Sheikh Saud al-Mojeb alisema kuwa uchunguzi wa kamati kuu ya ufisadi, ambayo inaongozwa na mwanamfalme wa umri wa miaka 32 Prince Mohammed Bin Salman unaendelea vyema.
Alitangaza kuwa watu 208 wameitwa kuhojiwa hadi sasa na kwamba 7 kati yao wameachiliwa.
No comments:
Post a Comment