Rais wa Marekani Donald Trump Jumapili amewaambia wanajeshi wa Marekani walioko katika kituo cha jeshi la anga cha Yokota, Japan kwamba “hakuna mtu yeyote, siyo dikteta, siyo serikali … asijaribu kudharau azimio la Marekani.”
Matamko yake yamekuja wakati akianza ziara yake itakayo mchukua takriban wiki mbili katika Bara la Asia ambayo itaangaza suala la Korea Kaskazini.
Baadhi ya ahadi zake, zikiwa zimeelekezwa kwa vikosi vya Marekani, zinaweza kutafsiriwa kama ni onyo lisilo la moja kwa moja kwa taifa ambalo limetengwa:
“Nyinyi ni tishio kubwa kwa madikteta na wakandamizaji ambao wanataka kuwaangamiza watu wasiokuwa na hatia.”
Ujumbe kwa Korea Kaskazini
Wakati akiwa njiani kuelekea Japan, rais amezungumza na waandishi wa habari akiwa katika ndege ya Air Force One, ambapo mwandishi wa VOA alimuuliza iwapo ana ujumbe kwa watu wa Korea Kaskazini.
“Nafikiri ni watu wazuri sana,” rais alisema. “Niwachapa kazi. Ni watu wakarimu, ni wakarimu kuliko vile dunia inavyowafahamu na kujua, ni watu wazuri sana. Na natumai kila kitu kitaenda sawa na kila mtu. Itakuwa ni jambo la kupendeza iwapo tutaweza kutatua hili kwa ajili ya watu hawa wema na kwa kila mtu.”
Trump pia amegusia kuwa anatarajia kukutana na Rais wa Russia Vladimir Putin pembeni ya mkutano wa viongozi wa APEC utakaofanyika baadae Ufilipino wakati wa ziara yake hii.
No comments:
Post a Comment