Thursday, November 16

Spika awataka mawaziri kusikiliza maswali ya wabunge



Spika wa Bunge, Job Ndugai
Spika wa Bunge, Job Ndugai 
Dar es Salaam. Spika wa Bunge, Job Ndugai amewataka mawaziri waache kupiga stori bungeni na kusikiliza wabunge wanapouliza maswali.
Ndugai ametoa agizo hilo leo Alhamisi asubuhi wakati wa kipindi cha maswali na majibu bungeni.
“Kipindi cha maswali waheshimiwa mawaziri acheni kupiga stori… waheshimiwa mawaziri hamsikilizi,’’ amesema Ndugai
Kauli ya Ndugai imekuja baada ya Mbunge wa Viti Maalum, Mwantumu Dau Haji kuuliza swali la nyongeza kuhusu kilimo cha umwagiliaji alilolielekeza kwenye Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira.
Wakati akiruhusu naibu waziri kujibu swali hilo, Spika amesema kuwa swali hilo lilipaswa kujibiwa na wizara ya maji hivyo kumtaka naibu waziri wa wizara hiyo kujibu.
“Hilo swali lilitakiwa liende Wizara ya Maji, Naibu Waziri Maji, Mh Aweso (Jumaa),” Ndugai alimtaka Naibu Waziri wa Maji kujibu swali na kuongeza kuwa, “ndo shida mnakuwa mnaongea, hamsikilizi humu ndani, jibu swali.”
Baada ya hapo, Spika alimwambia Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira na Muungano, Kangi Lugola kujibu swali hilo. “Mh Kangi Lugola okoa jahazi’ alisema Ndugai ambaye alikuwa akiwasisitiza mawaziri kuwa makini kusikiliza. 
Pia, Spika amewataka baadhi ya mawaziri kujiandaa kutoa majibu mafupi katika maswali yanayohusu wizara zao, “Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Afya, Wizara ya Maji kwa majibu yanayokuja na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa majibu yanayokuja, ni marefu sana mawaziri wawe wanatoa majibu kwa ufupi,” amesema

No comments:

Post a Comment