Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mwambapa leo Novemba 28 ametoa hukumu hiyo baada ya upande wa mashtaka kudhibitisha kesi pasipo kuacha shaka.
Ni baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi watano na utetezi uliotolewa na mshtakiwa mwenyewe.
Mshtakiwa, Mtozoma ambaye ni mkazi wa Magomeni Kagera alikuwa akikabiliwa na kesi ya kupatikana na silaha ambayo atatumikia kifungo cha miaka mitano jela.
Na katika shtaka la kupatikana na risasi pia atatumikia kifungo cha miaka mitano jela.
Wakili wa Serikali,Nassoro Katuga kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo ameomba mahakama itoe adhabu kali kwa mshtakiwa huyo ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.
Kwa mujibu wa kesi hiyo, mshtakiwa huyo Mtozoma anadaiwa kuwa Agosti 11,2016 katika eneo la Magomeni Kagera wilaya ya Kinondoni alikutwa akiwa na bastola moja aina ya Browing yenye kumbukumbu namba 90002 iliyosajiliwa kwa namba TZCAR-A222683 bila ya kuwa na leseni.
Mshtakiwa huyo anadaiwa kuwa Agosti 11,2016 katika eneo hilo la Magomeni Kagera wilaya ya Kinondoni alikutwa akiwa na risasi 6 bila ya kuwa na leseni.
No comments:
Post a Comment