Tuesday, November 7

Saudia yadai Iran ilihusika katika shambulio la kombora

Hatua hiyo inaimarisha hatua ya mwanamfalme Mohammed bin SalmanHaki miliki ya pichaEPA
Image captionHatua hiyo inaimarisha hatua ya mwanamfalme Mohammed bin Salman
Saudia imeongeza mashambulizi yake ya maneneo shidi ya Iran na washirika wake.
Imelishutumu kundi la wapiganaji wa Lebanon Hezbollah kwa vitendo vya uchokozi ambavyo imevitaja kuwa tangazo la vita.
Riyadh pia imeilaumu Tehran kwa shambulio la kombora siku ya Jumamosi lililolenga mji mkuu wa Saudia ambalo lilitekelezwa na waasi wa Houthi mjini Yemen.
Iran imekana madai hayo ikisema kuwa ni uchokozi wa kivita wa Saudia ambao unatishia amani katika eneo la mashariki ya kati.
Marekani imesema kuwa inaunga mkono msimamo wa Saudia dhidi ya Iran.
Rais Trump ambaye yuko mashariki mwa bara Asia pia alichapisha ujumbe wa Twitter akisema kuwa ana matumaini na hatua zinazochukuliwa na mfalme Salman na mwanamfalme Mohammed kukabiliana na ufisadi katika ufalme huo.
Siku ya Jumatatu mwanasheria mkuu wa Saudia alisema kuwa kukamatwa kwa wafanyikazi wakuu wa ufalme huu wiki hii ikiwemo mawaziri na wafanyibiashara ulikuwa mwanzo tu wa vita dhidi ya ufisadi.

No comments:

Post a Comment