Tuesday, November 7

Mpiga picha akamatwa Kenya akipiga picha shamba la Rais Kenyatta

Uhuru KenyattaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionUhuru Kenyatta
Mpiga picha mmoja wa shirika la kimataifa amekamatwa na kushtakiwa mahakamani Jijini Nairobi, baada ya 'kuzuru shamba la Kenyatta' bila idhini.
Shirika la habari la AFP, limesema kwamba, mpiga picha wake mkuu wa Afrika Mashariki, amefikishwa Jumatatu mahakamani nchini Kenya na kushtakiwa kwa kosa la kuingia kwenye shamba linalomilikiwa na familia ya Rais Uhuru Kenyatta.
Mpiga picha huyo raia wa Japan Yasuyoshi Chiba, mwenye umri wa miaka 46, alikamatwa siku ya Ijumaa kwenye shamba la kampuni ya maziwa ya Brookside dairy, inayomilikiwa na familia ya Rais wa kwanza wa Kenya na wa sasa Bw. Uhuru Kenyatta.
Alikuwa amekwenda huko kupiga picha ya nembo ya kampuni hiyo ya maziwa, baada ya muungano wa upinzani nchini humo-NASA, kutoa wito wa kususiwa kwa bidhaa zote za vigogogo wakuu wa chama tawala cha Jubilee zikiwemo bidhaa za Brookside, kufuatia kumalizika kwa uchaguzi mkuu enye utata wa Urais.

No comments:

Post a Comment