Picha za tembo wawili wanaoonekana wakiutoroka umati wa watu uliowachoma moto imeshinda tuzo kuu katika shindano la picha za wanyama pori.
Picha ya Biplab Hazra inaonyesha tembo mtoto akichomeka moto huku yeye na tembo mkubwa wakitoroka kwa kuhofia maisha yao mashariki mwa India.
Akitangaza tuzo hiyo, jarida la Sancuary lilisema kwamba unyanyansaji wa aina hii unafanyika mara kwa mara.
Picha hiyo ilichukuliwa magharibi mwa Bengal ambako migogoro kati ya wanyama na binaadamu imekithiri.
Haijulikani ni nini haswa kilichotokea kwa wanyama hao katika picha hiyo ilioshinda tuzo ambayo ilipigwa katika wilaya ya Bankura.
Wilaya hiyo imekuwa ikigonga vichwa vya habari kwa vifo vya binadamu vinavyotokana na mzozo na tembo.
Ujumbe huo ulisema ''Umati wa wanaume waliokuwa wakiwazomea tembo hao ulikuwa ukiwachoma'' wakati Biplab Hazra alipopiga picha hiyo.
Anakumbuka kelele za ndovu hao walipokuwa wakitoroka.
''Kwa wanyama hao wazuri ,wanaowavutia Jamii sasa wako katika hali ya mbaya'', aliongezea.
Picha hiyo imevutia wengi katika mitandao ya kijamii.
Mainak Mazumdar anayeishi Bankura, alisema kuwa wanakijiji ni wa kulaumiwa kwa kuharibu mazingira ya wanyama pori na kwamba tembo wamekuwa wakinyanyaswa ma kuteswa.
Lakini alisema tembo wamewatesa wanadamu kwa kuharibu mimea yao, mashamba na kuwaua wato wasio na hatia
No comments:
Post a Comment