Saturday, November 25

Oscar Pistorius aongezewa miaka 13 jela

Oscar Pistorius aongezewa miaka 13 jelaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionOscar Pistorius aongezewa miaka 13 jela
Mahakama ya Afrika Kusini imemuongezea hukumu ya miaka 13 na miezi sita jela mwanariadha mlemavu wa Afriika Kusini kwa kumuua mpenziwe .
Waendesha mashtaka wanasema kuwa kifungo cha miaka sita alichopewa mwanariadha huyo kwa kumuua Reeva Steenkamp kilikuwa hafifu mno.
''Wazazi wa Bi Steenkamp walijawa na hisia wakitazama hukumu hiyo nyumbani wakati ilipokuwa ikitolewa'' , msemaji wao alisema.
Wanahisi kwamba sasa haki ya mwana wao imefanyika .
''Sasa anaweza kulala mahali pema peponi'', Tania Koen aliambia chombo cha habari cha Ap.
''Lakini wakati huohuo , watu wanahisi kwamba wamefika mwisho , uweli ni kwamba wataishi na majonzi ya kumpoteza Reeva kila siku'', alisema bi Koen.
Oscar Pistorius alidai kwamba alimpiga risasi Reeva Steenkamp siku ya wapendanao 2013 baada ya kudhani alikuwa mwizi.
Rufaa ya mahakama ya juu mjini Bloemfontein imempatia Pistorius kifungo kisichopungia miaka 15 kwa mtu ambaye ameua nchini Afrika Kusini huku akiwa amehudumia miaka michache tayari.

No comments:

Post a Comment