Saturday, November 25

Emmerson Mnangagwa ni nani?

Mfahamu rais mpya wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa
Image captionMfahamu rais mpya wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa
Bwana Emerson Mnangagwa amekuwa mwandani wa Robert Mugabe kwa karibu miaka 40 tangu na hata kabla Zimbabwe kujipatia uhuru wake.
Bwana Mnangagwa mwenye umri wa miaka 75 amekuwa karibu zaidi na Mugabe tangu enzi zile wakiwa jela walipokamatwa kutokana na harakati zao za kupigania na katika shughuli nzima za mapambano ya kuikomboa Zimbabwe.
Bwana huyo alizaliwa tarehe 15 septemba mwaka 1942 kabla ya babake kuhamia nchini Zambia alikoanza harakati za mapambano.
Safari yake ya kufikia hadi sasa anaapishwa kuwa rais wa Zimbabwe imekuwa ya utaraibu lakini ya kiuhakika.
Uhuru ulipopatikana , bwana Mugabe hakumsahau rafiki yake alimchaguwa kuwa waziri wa Usalama wa kitaifa .
Lakini baadae aliteuliwa kushikilia nyadhifa mbali mbali katika serikali ya rafiki yake na babake wa kisiasa - Robert Mugabe.
Lakini safari yake hadi kufikia kuchagulikwa kuwa naibu rais mwaka 2014 haikuwa rahisi .
Kuna wakati alipokukuwa akikosana na bwana Mugabe na mara kushushwa madaraka na mara nyegine kukumbukwa na kupandishwa tena cheo.
Kwa mfano mwaka 2004 Mnangagwa alifutwa kama katibu mkuu wa chama tawala cha ZANU-PF kwa madai eti alikuwa ananyemelea cheo cha naibu rais wa Zimbabwe.
Lakini mambo yalianza tena kumuendea vizuri pale mwaka wa 2008 alipochaguliwa na bwana Mugabe kuongoza kampeni yake ya Urais.
Inasadikiwa kwamba bwana Mugabe aliopteza duru ya kwanza katika uchaguzi huo kwa kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai.
Lakini wakati kura ya marudio ilipotangazwa tena , inasadikiwa kwamba bwana Mnangagwa aliongoza fujo na mashambulizi dhidi ya viongozi wa upinzani pamoja na wafuasi wao hivyo kumfanya upinzani wake mkuu Morgan Tsvangirai kususia kura hizo na kumfanya Mugabe achaguliwe tena kama rais.
Ni hapo ndipo nyota yake ilianza kung'ara tena
Na pale Mnangagwa alipofutwa kazi kama naibu rais wengi walitabiri kwamba , mamba huyo ameliwa na Bi Grace Mugabe ,mke wa Robert Mugabe lakini sasa amerudi na kuchukua wadhifa wa rais mpya wa Zimbabwe.

No comments:

Post a Comment