David Lyimo, anayeuguza ndugu yake katika taasisi hiyo aliliambia gazeti hili jana: “Taarifa ambazo awali tulikuwa tukizisikia kuhusu kero ya dawa hapa kwa sasa hatujazikuta, mgonjwa wangu anapatiwa dawa, ni aina moja tu tunayotakiwa kununua lakini mionzi na dawa zingine tunapata hapa.”
Akizungumza na watendaji wa taasisi hiyo na Bohari ya Dawa (MSD), mkurugenzi mtendaji wa ORCI, Dk Julius Mwaiselage alisema upatikanaji dawa, vifaatiba na vitendanishi ilikuwa tatizo katika utendaji na changamoto kwa wagonjwa ambao walilazimika kununua kwa bei ghali.
Dk Mwaiselage alisema bajeti ya taasisi hiyo mwaka 2015 ilikuwa ni Sh790 milioni, sasa ni Sh7 bilioni huku ikiwa na akiba ya Sh4.3 bilioni za dawa.
Naye mkurugenzi mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu alisema taasisi hiyo inatambua dawa za saratani ni ghali lakini atahakikisha zinaendelea kupatikana kwa wakati ili kuokoa maisha ya Watanzania.
“Ocean Road ni mteja muhimu, hivyo nipo tayari muda wote kuwahudumia leteni orodha ya mahitaji ya dharura hata leo,” alisema.
Katika ziara hiyo, Bwanakunu alitembelea hospitali za Amana, Mwananyamala na Sinza Palestina.
No comments:
Post a Comment