Shirika la habari la AFP limeripoti kuwa Robinho alishiriki katika ubakaji huo Januari mwaka 2013 wakati akiichezea klabu ya AC Milan inayoshiriki Ligi Kuu ya Italia, maarufu kwa jina la Serie A.
Robinho, ambaye ameichezea timu ya taifa ya Brazil michezo 100, alipatikana na hatia ya kubaka msichana mwenye umri wa miaka 22 ambaye ni raia wa Albania. Hata hivyo, nyota huyo wa zamani hakuwepo kortini.
Watu wengine watano pia walishtakiwa kwa kosa hilo, lakini hukumu yao bado haijajulikana.
AFP imekariri gazeti la kila siku la jijini Milan, Corriere della Sera, likisema kuwa Robinho na marafiki zake watano walimlewesha msichana huyo "kiasi cha kutojitambua na hivyo kutoweza kuwakatalia".
Baadaye walichangia kufanya naye ngono kwa kuachiana.
No comments:
Post a Comment