Monday, November 6

Nyaraka za Paradiso: Waziri wa uchumi Marekani ashutumiwa

Wilbur Ross ametekeleza mchango muhimu katika maisha ya Trump ya kibiashara na kisiasaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWilbur Ross ametekeleza mchango muhimu katika maisha ya Trump ya kibiashara na kisiasa
Waziri wa uchumi nchini Marekani Wilbur Ross ameshutumiwa kwa kuwapotosha maseneta nchini humo baada ya nyaraka kuonesha ana uhusiano na Urusi.
Nyaraka hizo ambazo zimefichuliwa, ambazo zinafahamika kama Nyaraka za Paradiso, zimeonesha kwamba amekuwa wakijihusisha na kampuni ambayo ina uhusiano wa kifedha na serikali ya Urusi.
Seneta wa chama cha Democratic Richard Blumenthal ameambia NBC kwamba uhusiano huo ni wa kushangaza.
Nyaraka hizo ambazo zimekabidhiwa kundi la mashirika ya habari, ikiwemo BBC, zinaonesha Bw Ross aliendelea kuwa na maslahi katika kampuni ya usafirishaji wa mafuta na gesi iliyokuwa ikihudumia kampuni ya kawi ya Urusi, Sibur.
Wawili kati ya wamiliki wa kampuni hiyo wamewekewa vikwazo na Marekani na mwingine ana uhusiano wa karibu sana na Rais Vladimir Putin.
Seneta Blumenthal amesema Bw Ross aliambia Bunge la Congress kwamba hakuwa tena na hisa katika kampuni hiyo kwa jina Navigator.
Wizara ya uchumi Marekani imesema Ross hakufanya jambo lolote ambalo ni kinyume cha sheria na kwamba hajawahi kukutana na Warusi hao ambao wamewekewa vikwazo na Marekani.
Graphic - Wilbur Ross; The Russian Connection

No comments:

Post a Comment