Mwanamfalme mmoja nchini Saudi Arabia amefariki baada ya helikopta aliyokuwa akisafiria kuanguka karibu na mpaka wa nchi hiyo na yemen, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti.
Mwanamfalme Mansour bin Muqrin, naibu gavana wa mkoa wa Asir, alikuwa akisafiri pamoja na maafisa kadha wa serikali helikopta hiyo ilipoanguka, runinga ya Al-Ikhbariya imesema.
Chanzo cha ajali hiyo hakijabainika.
Saudi Arabia ilisema ilitungua kombora la masafa marefu lililokuwa limerushwa kutoka Yemen likiwa karibu na uwanja wa ndege wa Riyadh Jumamosi.
Pia, wikendi, watu wengi wakiwemo wana wafalme 11 na mawaziri wanne walikamatwa katika kampeni ya kukabiliana na rushwa ambayo inatazamwa kama njama ya kuimarisha mamlaka ya mrithi mtarajiwa wa ufalme.
Taasisi hiyo ya kukabiliana na ufisadi iliundwa na mwanamfalme wa kwanza kwenye urithi Mohammed bin Salman.
Mwanamfalme Mansour bin Muqrin, aliyefariki, ni mwana wa mwanamfalme aliyekuwa wa kwanza katika urithi awali.
Babake, Muqrin bin Abdul Aziz, alitengwa na ndugu wa kambo wa Mfalme Salman miezi kadha baada yake kurithi ufalme mwaka 2015.
Shirika la habari la Okaz limesema taarifa ambazo hazijathibitishwa zinasema hakukuwa na manusura kwenye ajali hiyo ya ndege.
No comments:
Post a Comment