Akizungumza leo Novemba 11, kwenye ufunguzi wa kampeni hizo Kimara Suka jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe amesema amempokea Nyalandu na ataungana naye kwenye mkutano mwingine kama huo utakaofanyika Mtwara mjini hapo kesho.
‘’Kila anayeondoka chama tawala anaitwa fisadi, potelea mbali wamempokea na wengine wengi watahamia kuleta mabadiliko’’ amesema na kuongeza
"Mabadiliko hayaji ghafla yanakuja taratibu na ujio wao ndiyo mwanzo wa mabadiliko tulipoanza na tulipo sasa kuna tofauti kubwa" amesema Mbowe.
Amefafanua kwamba haungi mkono nchi kuwa na wezi, lakini anashauri sheria iachwe iamue haki badala ya kuingiliwa kama inavyofanyika kwa mahakama.Huku akidai kwamba watawala wana hofu ndiyo maana hawataki ushauri.
Amesema wataendelea kupigania haki ya kupigania haki ya kufanya mikutano ya kisiasa na ipo siku wataingia mtaani kuidai bila kuogopa vifaru.
Amesema huu siyo wakati wa kuogopa na kukaa kimya ni wakati wa kusimama na kutetea haki ya kufanya siasa.
Kuhusu uchumi kusinyaa amesema ni kweli umesinyaa na inaonekana wazi jinsi maisha yalivyo wananchi, wafanyabiashara, watawala wote wanalia njaa hakuna mwenye nafuu.
Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob amesema anahitaji kuongeza nguvu ya kuleta maendeleo katika manispaa hiyo, hivyo mgombea udiwani kata ya Saranga Ephram Kinyafu anatosha.
Naye Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani Frederick Sumaye amehoji kuhusu hali za wananchi kuendelea kuwa mbaya.
"Tumeamua na tunamaanisha wakati huu ushindi ni lazima, na mtakaotupa ushindi ni nyie wananchi" amesema Sumaye.
No comments:
Post a Comment