Ng’ombe hao walikamatwa baada ya kufanyika operesheni ya kuzuia mifugo kuingizwa nchini kwa njia ya magendo.
Kati ya idadi hiyo, ng’ombe 572 wapo Kijiji cha Kumuhasha na 350 wapo Kijiji cha Busunzu.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari katika Kijiji cha Kumuhasha, Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Louis Bura alisema walibaini ng’ombe hao kwa kuwa wamepigwa chapa ya nchi hiyo.
Alisema wamiliki wa ng’ombe hao walilazimika kutafuta sehemu nyingine ya malisho ili kuokoa mifugo yao.
“Ndipo wamiliki hao walipovamia pori la akiba la Muyowosi na kuanza kuchungia ng’ombe humo, lakini hawakujua kwamba mkono wa Serikali ni mrefu na hatimaye tuligundua wameficha ng’ombe kwenye pori hilo, tumewakamata na tunashikilia mifugo yao,” alisema Bura.
Ng’ombe hao walipitia pori la Burigi lililopo mkoani Kagera kabla ya kutoroshwa huko na kuingizwa pori la Muyowosi lililopo Kibondo.
Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Juma Mnwele alisema hawapo tayari kuona wafugaji wakiigeuza halmashauri kama kichaka cha kuficha mifugo kutoka nchi jirani na mikoa mingine nchini.
Alisema endapo wamiliki wa ng’ombe hao watashindwa kulipa fidia ndani ya siku tatu mifugo hiyo itauzwa kwa mnada.
Makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Hamisi Kapukii alisema kuingiza mifugo kiholela kunasababisha mapigano baina ya wakulima na wafugaji kwa vile mifugo huharibu mazao.
Mkazi wa Kijiji cha Kumuhasha, Noel Joel alisema mifugo imekuwa ikiharibu mazao yao.
No comments:
Post a Comment