Sunday, November 5

Mvua kubwa kuendelea kunyesha nchini


Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania imetoa tahadhari ya mvua kubwa katika baadhi ya mikoa kuanzia saa 3:00 usiku wa leo.
Kupitia utabiri wa hali ya hewa wa saa 24 zijazo baadhi ya mikoa inatarajia kuathirika na  vipindi vifupi vya mvua kubwa.
Baadhi ya maeneo katika mikoa ya Kagera, Geita, Mara, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Kigoma, Tabora, Katavi na Rukwa imeombwa kuchukua tahadhari ya mvua hizo.
Kupitia matazamio, mvua hizo zinaonekana kuendelea hadi Novemba 7 katika Ukanda wa ziwa victoria na Magharibi mwa nchi.

No comments:

Post a Comment