Aliyekuwa kiongozi wa Catalonia Carles Puigdemont na waliokuwa washauri wake wanne wamejisalimisha kwa polisi nchini Ubelgiji, kwa mujibu wa msemaji wa mkuu wa mshtaka.
Alisema kuwa jaji ataamua Jumatatu ikiwa atatekeleza waranti wa kukamatwa uliotolewa na jaji nchini Uhispania siku ya Ijumaa.
Bw Puigdemont alikimbia kwenda Ubelgiji baada ya ya Madrid kuchukua udhibiti kamili wa Catalonia kufuatia kura ya maoni ya uhuru.
Amesema kuwa atarudi nchini Uhispania ikiwa atahakikishiwa kupata hukumu iliyo ya haki.
Yeye pamoja na washirika wake wanne wanatafutwa kwa mashtaka ya uasi, uhaini na matumizi mabaya ya pesa za umma kufuatia kura ya maoni ambayo mahakama ya Uhispania iliitanga kuwa iliyo kinyume na sheria.
Wiki iliyopita waziri mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy alitangaza udhibiti maalum kwa Catalonia, ambapo alivunja bunge la eneo hilo na kuitisha uchaguzi wa mapema.
Washirika wenegine wa Bw, Puigdemont walio kuzuizini ni pamoja na Meritxell Serret (waziri wa zamani wa kiliimo), Antoni Comín (Waziri wa zanai wa afya),Lluís Puig (waziri wa zmania wa utamaduni) na Clara Ponsatí (waziri wa zamnai wa elimu).
No comments:
Post a Comment